Onesimo Nesib

Picha na sahihi zake halisi.

Onesimo Nesib (kwa Kioromo: Onesimoos Nasiib; 1856 hivi – 21 Juni 1931) alikuwa Mworomo aliyejiunga na madhehebu ya Walutheri (31 Machi 1872) akawa mmisionari nchini Ethiopia akatafsiri Biblia ya Kikristo katika Kioromo. Hivyo amekuwa mwanzilishi wa fasihi ya Kioromo ya kisasa[1].

Onesimo Nesib anatazamwa kama mtakatifu katika Lutheran Book of Worship ya Marekani.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 21 Juni.

  1. Fighting Against the Injustice of the State and Globalization: Comparing the African American and Oromo Movements p.73. Asafa Jalata, 2001

© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search